Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoani Mtwara imemfutia shtaka la kesi ya uchochezi iliyokuwa ikimkabili Mbunge wa Mtwara Mjini (CCM) Hassnein Murji.
Katika mahakama hiyo wakili anayemtetea mbunge huyo Peter Kibatala aliiomba mahakama kuifuta kesi hiyo ambayo ilisomwa Julai 3, mwaka huu kwa madai kwamba hati ya mashtaka haionyeshi ni makosa yapi mtuhumiwa aliyatenda kabla ya kukamatwa.
Murji alifikishwa kwa mara ya kwanza mahakamani hapo akikabiliwa na kesi ya uchochezi baada ya kudaiwa kufanya makosa hayo Januari 19, mwaka huu katika eneo la Ligula mkoani hapa.
Kutokana na hoja ya wakili Kibatala, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo Dynes Lyimo alifuta shtaka hilo na kumwachia mshtakiwa huru.
CHANZO:habarimasai.com