MABINTI WALIOMWAGIWA TINDIKALI ZANZIBAR WANAENDELEA VIZURI

 
Imeripotiwa kutoka London – Uingereza kuwa mabinti wawili ambao walimwagiwa tindikali Kisiwani Unguja ambapo walikwenda kama wafanyakazi wa kujitolea kufundisha kiingereza mashuleni wanaendelea vizuri.

Kwa sasa mabinti hao wanatibiwa katika hospitali ijulikanayo kwa jina la Chelsea and Westminster ambayo imebobea kwenye kutibu matatizo yanayotokana na kuunguzwa mjini London.

Mama yake Katie, mmoja wa majeruhi hao, ajulikanaye kwa jina la Nicky Gee amesema familia zao zimekuwa zinapitia katika kipindi kigumu sana kufuatia unyama ambao mabinti wao wametendewa wakati wakiwa wanafanya shughuli za kujitolea visiwani Zanzibar.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo