Mkuu
wa Kitengo cha Huduma za Dharurua 'Emergency Medicine Profesa, Victor
Mwifongo kushoto akibadilishana namba za mawasiliano na Meneja wa
Kanda ya Afrika Mashariki wa kampuni ya Chloride Exide Bw,Gabriel
Ondoyo Mratibu wa Masoko wa Kampuni hiyo Bw, Robert Hiza
Na Mwandishi Wetu
MRATIBU wa Masoko wa Kampuni ya Chloride Exide Bw, Robert Hiza leo
ametoa msaada wa Betri mbili katika kitengo cha Emergency Medicine ya
hospitali ya Taifa Muhimbili .
Msaada huo wa kwanza kutoa
inaendana na miaka 50 ya kampuni hiyo ambapo watatoa viti mbalimbali
katika hospital za Serikali vikiwemo Sola kwa ajili ya umeme wa jua .
Akipokea msaada huo.Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Dharura 'Emergency
Medicine Profesa, Victor Mwifongo amewashukuru kampuni ya Chloride
Exide kwa kuliona hilo kwani ni mara ya kwanza katika kitengo chao
kupokea msaada kama huo, na kuwaomba wadau wengine kujitokeza kusaidia
vitu mbalimbali ikiwemo hata magari kama yapo tunaomba msaada maana
hapa kitengo chetu ni cha mambo ya dharura na kinategemewa sana kama
mnavyojua alisema Prof Victor Mwifongo
Nae Mkuu wa Madereva wa Kitengo cha Emergency Medicine Bw. Kafuru
Rashidi amendelea kutoa shukrani kwa kampuni hiyo kwa kuliona hilo
kwani yeye kama Dereva ameona ni jambo bora sana
|