KIPA namba moja wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' aliyekuwa
mlinda mlango wa kutumainiwa wa klabu ya Simba SC, Juma Kaseja, leo
asubuhi ameungana na wachezaji wa Mtibwa Sugar kufanya mazoezi kwenye
Uwanja wa Chuo cha Ustawi wa Jamii uliopo Kijitonyama jijini Dar es
Salaam.
Katika mazoezi hayo Kaseja alikutana na mshambuliaji Musa Hassan Mgosi ambaye aliwahi kucheza naye Simba SC.
Mgosi kwa sasa ni mchezaji wa Mtibwa Sugar wakati Kaseja bado hatma yake haijafahamika baada ya kuachana na Simba msimu uliopita.
(PICHA NA RICHARD BUKOS / GPL)