Jeshi
la polisi nchini limepokea msaada wa gari maalum lenye mitambo
itayoweza kufanya upelelezi,ukaguzi na uchunguzi wa kitaalam
utakaosaidia kupata ushahidi wa uhakika katika kupambana na matukio ya
uhalifu hapa nchini.
Akiziungumza na waandishi wa habari, baada ya kusaini hati za
ushirikianao wa jeshi la polisi la Uturuki na kisha kukabidhiwa gari
hilo, mkuu wa jeshi la polisi nchini,insepekta jenerali Saidi Mwema
amesema baadhi ya wahalifu wamekuwa wakihachiwa huru na mahakama kwa
sababu ya ushahidi wa jeshi la polisi kutokamilika kutokana kutokuwepo
na vifaa vya kitaalam ambapo amesisitiza vifaa vilivyomo katika gari
hilo vitasaidia kukusanya taarifa za uhakika za matukio ya uhalifu.
Naibu mkurugenzi wa jeshi la polisi la taifa la uturuki bwana Zeki
Gakatalilaya amesema makubalino ya ulinzi ni moja ya njia ya
kushirikiana yatakayosaidia majeshi la polisi katika nchi hizo
mbali,ambapo amesema tayari serikali ya Uturuki inashirikiana na nchi
zaidi ya tisa katika maswala ya usalama.
Naibu katibu mkuu wa wizara ya mambo ya ndani bibi Mwamini Malemi
amesema kukabidhiwa kwa gari hilo ni mwendelezo wa makubaliano kati ya
rais Jakaya Kikwete na rais wa Uturuki ya kuendeleza jeshi la polisi la
Tanzania na Uturuki katika kuangalia matukio ya kiharifu na kufanya
uchunguzi wa kitaalam na kuondokana na tatizo la ushahidi kutokakamilika
kwenye vyombo vya utoaji haki.
chanzo:itv