HIVYO NDIVYO WACHEZAJI WA ZAMANI WA KLABU YA RELI, PAN AFRIKA NA COAST UNION NAMNA WALIVYOMZIKA IDRISA NGURUNGU MOROGORO

Juma Mgunda kulia akiongea jambo na Hussein Ngurungu mara baada ya mazishi ya mdogo wake Idrisa Ngurungu aliyefariki kwa ajali ya gari katika barabara kuu Morogoro-Kisaki eneo la Kibungo siku ya ijumaa Agosti 2 mwaka huu mkoani Morogoro na kusababisha watu wawili kufariki dunia papo hapo na wengine wanee kujeruhiwa vibaya katika ajali hiyo iliyotokea majira kati ya saa 6 na saa 7 mchana mkoani Morogoro.
Jeneza lenye mwili wa mchezaji nyota wa zamani aliyewahi kuzichezea klabu za Reli ya Morogoro, Pan Afrika ya Dar es salaam na Coastal Union ya Tanga, ldrisa Ngurungu kulia na la Laila Mgoto yakiwa katika makaburi ya Kola muda mfupi kabla ya mazishi yao baada ya kuf
ariki dunia katika ajali ya gari barabara kuu Morogoro-Kisaki eneo la Kibunge siku ya ijumaa agosti 2 mwaka huu mkoani Morogoro.Jeneza lenye mwili wa mchezaji nyota wa zamani aliyewahi kuzichezea klabu za Reli ya Morogoro, Pan Afrika ya Dar es salaam na Coastal Union ya Tanga, ldrisa Ngurungu kulia na la Laila Mgoto yakiwa katika makaburi ya Kola muda mfupi kabla ya mazishi yao baada ya kufariki dunia katika ajali ya gari barabara kuu Morogoro-Kisaki eneo la Kibunge siku ya ijumaa Agosti 2 mwaka huu mkoani Morogoro.
Huyu ni mchezaji wa zamani wa klabu ya Pan Afrika na Yanga Baakari Malima (Jembe Ulaya) katika mazishia hayo ambapo Malima aliwahi kucheza na Idrisa Ngurungu katika klabu ya Pan Afrika miaka hiyo.
Kocha John Simkoko naye akizungumza jamba na mmoja watu walioshiriki katika mazishi hayo.
 Jeneza la dada yetu mpendwa Laila Mgoto likiingizwa katika gari mara baada ya sala ya mwisho katika msikiti wa Mjipya tayari kwa kuanza safari ya kuelekea katika makaburi ya Kola kwa mazishi.
Sehemu ya usafiri wa pikipiki waliotumia watu mbalimbali kuwasafirisha kutoka nyumbani kwa marehemu hadi makaburi ya Kola kwa ajili ya kushiriki mazishi hayo.
Magari yakielekea Kola katika mazishi hayo eneo la Kilima kwa Mnyonge Kilakala.PICHA NA DJ SEK BLOG


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo