Mdhibiti
na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Bw. Ludovick S.L. Utouh
amekutana na Waandishi wa Habari katika Ukumbi wa Ubungo Plaza jijini
Dar es Salaam ambapo ametoa ufafanuzi kukanusha tuhuma zilizotolewa
katika baadhi ya vyombo vya habari vikimnukuu Mbunge wa Kigoma Kaskazini
Mhe. Zitto Zuberi Kabwe ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya PAC
kwamba, kuna ufisadi katika matumizi ya fedha zilozotolewa katika bajeti
ya 2011/2012 kwa ajili ya mradi maalum wa barabara unaosimamiwa na
Wizara ya Ujenzi.
Bw. Utouh amebainisha kwamba kiasi cha Shs. 252,975,000 kilichohojiwa
na ukaguzi ni fedha ambazo zimeonyeshwa kwenye taarifa za hesabu za
Wizara kama ni miradi mipya ya mwaka 2011/2012 tofauti na uhalisia
wenyewe ulivyo.
Serikali katika dhamira ya kuimarisha mtandao wa barabara nchini,
iliweka kwenye bajeti yake ya mwaka wa fedha 2011/12 Kasma maalum ya
ujenzi wa miradi ya barabara na kuitengea jumla ya shilingi
252,975,000,000.00 kwa ajili ya kulipia kazi za barabara zinazoendelea.
Fedha zote zilitolewa na HAZINA kwa madhumuni hayo na kwa kufuata
taratibu za Serikali.
Wizara ya Ujenzi kupitia TANROADS ililipia kazi
hizo za barabara kwa maana ya madai ya Wakandarasi na Wahandisi Washauri
wa miradi mbalimbali inayoendelea.
"Hivyo katika kujadili hesabu za Wizara ya Ujenzi hakukuwepo na tuhuma
zozote za ufisadi ila Kamati ilimtaka Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu
za Serikali kuihakikishia matumizi ya fedha hizo jambo ambalo
litafanyika" alielezea Bw. Utouh.
CAG katika hatua nyingine alichukua fursa hiyo kuipongeza Wizara ya
Ujenzi kwamba inafanya kazi nzuri sana ya kusimamia na kujenga barabara
katika kona zote za nchi yetu.
Tuwapongeze kwa kazi nzuri wanayoifanya
ili wawe na moyo wa kuchapakazi zaidi kwa maendeleo ya nchi yetuâ€
alisistiza Bw. Utouh.