pilikapilika za jiji, Kwa bahati mbaya kama mnavyoelewa mambo ya familia haswa mke na mume siku hazifanani some time no some time yes!
Basi kwa mujibu wa mtu
wa karibu alivyoiambia blog hii ni
kwamba D'Jaro Arungu alivyokwaruzana na shemeji yetu (Mkewe) Aliamua
kujiondokea eneo la tukio na kwenda kutembea bila kujua aendako kutokana
na Hasira yaani alivurugwa! Katika matembezi yake yalikomea KBC night club
njia panda ya Airpot, Mtangazaji huyo alipaki gari lake Aina ya RAV 4 na
kuingia ndani ya Pub hiyo akaanza kupata moja mbili tatu, Siunajua tena
gambe? Mara akashangaa mang'amung'amu yani asubuhi kumekucha gafla bila
kuelewa kumekuchakucha vipi?''!
Ndipo alipoihirisha zoezi la moja mbili
tatu na kutoka nje, Du! inasikitisha sana kwamba alipofika kwenye gari
alifungua mlango wa gari lake kama kawaida na kuchomeka ufunguo kujaribu
kuwasha hola! Washa tena holaaa! Anashangaa linapiga King'ora yani alam
twiu! twiu! twiuuuuuuu!.., Ikabidi azime kwanza kutazama nini tatizo,
Mara kutazama akakuta milango ilichokonolewa kumbe wezi walishaanza
kufanya yao na walifanikiwa kuiba Redio ya gari na traksut ya mazoezi
iliyokuwemo humo, Mbali na hivyo kumbe katika harakati za kukwanyua Redio
wezi hao walikata baadhi ya nyaya ambazo zimepelekea gari la mtangazaji
huyo kugoma kuwaka.. na Blog hii ilimtafuta D'Jaro Arungu
kwanjia ya simu ya kiganjani kuweza kupata ukweli wa mambo, Kutokana na
makelele yaliyokuwepo katika eneo la tukio ilibidi mawasiliano yao
yafanyike kwa njia ya ujumbe mfupi kama mnavoona pale juu..
Jamani
kinamama punguzeni hasira kwenye ndoa zenuuuu!!! Mbali na yote na Blog hii rafiki na wewe inakupa pole sana ndugu D'Jaro a.k.a Baba Mzazi, Usiofu
punguza mawazo ni mitihani tu katika maisha kaka.
credits mdau:masainyotambofu.blogspot.com