
Bi. Hindu mwigizaji wa filamu Swahiliwood.
MWIGIZAJI wa filamu na Mtangazaji wa Redio, Chuma Suleiman ‘Bi. Hindu’
amemshukia mwenyekiti wa timu ya Simba Mh. Aden Rage kwa kusema kuwa ni
dikteta na anaendesha club hiyo kwa kuvunja katiba ya timu hiyo, msanii
huyo mkongwe katika tasnia ya filamu alisema kuwa Rage kama mwenyekiti
aliwahita wakitegemea kuelezea maendeleo ya timu yao ya Simba lakini
alichofanya ni kuwaonyesha makaratasi akidai ni katiba Bi. Hindu
akauliza je kila siku watakuwa wakitengeneza Katiba?

Bi. Hindu akiwa katika pozi lake.

Bi. Hindu msanii wa filamu Bongo.
“Yule Bwana Rage anatupeleka peleka tu, badala ya kutuambia vitu vya
msingi analeta porojo, ukimuuliza eti Katiba inampa mamlaka, katuletea
Polisi ili atutishe, polisi apeleke kwenye siasa za chama chetu cha CCM
na sio kwenye Simba yetu, Sikupenda hata ule mpangilio wa maswali, watu
wenye hoja nzito alikuwa akiwakataa na kuchagua wa kwake aliowapanga,”
alisema Bi Hindu.
Bi. Hindu alisema kuwa Mh. Rage anatakiwa akumbuke kuwa wakati
anaingia kuomba ridhaa ya kuongoza katika Club hiyo hakuja na Polisi
hivyo wanachama walimchagua ili alete maendeleo ya timu hiyo na siyo
ubabaishaji ambao ameonyesha katika cluba hiyo na sasa anaingiza siasa
badala ya kutatua matatizo yanayoidumaza Timu yao ya Simba.

Bi. Hindu mwigizaji wa filamu na mwanachama wa timu ya Simba.
Hivi karibuni Wanachama wa Timu ya Simba walifanya mkutano katika
Hoteli ya Star Light Mnazi Mmoja jijini Dar na kuung’oa uongozi wa klabu
hiyo uliopo madarakani chini ya Mwenyekiti wake, Ismail Aden Rage
kufuatia mwenendo mbaya wa timu yao.
Wanachama hao wamekabidhi uongozi wa klabu hiyo kwa Makamu Mwenyekiti
wa Kamati ya Fedha, Rahma Kharus ‘Malkia wa Nyuki’ na kumrudisha
kiongozi aliyejiuzulu hivi karibuni, Zacharia Hans Poppe, Wanachama hao
wamesema wanatarajia kuitisha mkutano mkuu na kuwachagua viongozi wapya
baada ya kumalizika kwa Ligi Kuu inayoendelea ili kuepusha kuivuruga
timu.
Chanzo cha Habari www.globalpublishers.com