Natasha akiwa na Neeema msimamizi wa Harusi yake.
Natasha akiwa katika shera.
Baada ya harusi hiyo ya kipekee kufungwa na kuhudhuriwa na waheshimiwa mbalimbali wakiwepo wasanii, maharusi walitoka na kuelekea Hotelini kwa ajili ya upigaji wa picha sambamba na kupumzika kabla ya kwenda ukumbini kwa ajili ya kusherekea ukumbi wa kisasa wa Magereza uliopo Ukonga.
Mr & Alex walipendeza kupita maelezo kwani kitu kilichowafanya wapendeze zaidi ilikuwa ni tabasamu lao sambamba na mavazi waliyovaa kwa siku hiyo maalumu kwao na kwa marafiki zao waliofika kwa kumsupport Natasha kama rafiki kipenzi wa jamii nzima ya tasnia ya filamu Swahiliwood, walipendeza sana na kuandika Hitoria ya maisha mapya.
Maharusi wakiwa katika nyuso za furaha na Rais wa TAFF Mwakifwamba.
Monalisa akiwa na wapambe wajukuu.
Natasha akiwa na Neema msimamizi wake.
Uongozi wa FC unatoa pongezi kwa maharusi wetu Mr & Mrs Alex kwa kuungana na kuwa mwili mmoja na si wawili tena, Mungu abariki maisha yao ya ndoa Takatifu iliyofungwa na Mungu. Ameni.
Natasha ni kiungo muhimu sana katika tasnia ya filamu Swahiliwood kwa mawasiliano na mwongozo pia kwa wasanii wote.
Ceo FC Myovela M.