AKAMATWA NA NGOZI YA CHUI MKOANI KATAVI

Jeshi la polisi Mkoa wa Katavi  linamshikilia Chelehani Kulwa 33 mkazi wa kijiji cha Kapanga Tarafa ya Mwese Wilaya ya Mpanda kwa tuhuma za kukamatwa na nyara za serikali ngozi ya chui 
 
Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari alisema  mtuhumiwa alikamtwa  hapo Agosti 1 mwaka huu majira ya saa tisa na nusu alasiri  nyumbani  kwake  akiwa na ngozi hiyo ya chui 
 
Kamanda Kidavashari alisema  mtuhumiwa alikamatwa na nyara hiyo ya Serikali kufuatia taarifa zilizolifikia jeshi la polisi  kuwa mtuhumiwa huyo  amekuwa akijishughulisha na uwindaji haramu na amehifadhi ndani ya nyumba yake ngozi ya chui 
 
Baada ya taarifa hizo kutoka kwa raia wema jeshi la polisi lilianza  uchunguzi  wa kumfuatilia mtuhumiwa huyo  kwa kushirikiana na wananchi wa kijiji hicho    cha Kapanga 
 
Kidavashari alieleza kuwa ndipo siku hiyo ya tukio polisi  walipokwenda kumpekua mhuhumiwa  Chelehani  nyumbani kwake na kumkuta na ngozi ya chui  yenye thamani ya shilingi  milioni  5.670,000 kinyume  cha sheria 
 
Alisema mtuhumiwa baada ya mahojiano  na jeshi la polisi alikiri kumiliki nyara hiyo ya Serikali kinyume na taratibu za sheria ya nchi 
 
Upelelezi wa tukio hili umeisha kamilika na mtuhumiwa anatarajiwa kufikishwa mahakamani mapema wiki ijalo ili aewze kujibu shitaka la kukamatwa na nyara za serikali kinyume cha sheria ya Jamhuri ya  muungano wa Tanzania  ambayo  inakataza mtu binafusi kumiliki nyara za Serikali
 
Na Walter Mguluchuma, Mpanda


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo