AJINYONGA BAADA YA KUFELI MTIHANI WA UALIMU

Na Diana Rubanguka, Kigoma.
MWANAFUNZI wa chuo cha Ualimu Tabora amekutwa amejinyonga katika eneo la Burega lililopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji Mkoani Kigoma.
 
Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma Freisser Kashai amesema kuwa mnamo Julai 31 mwaka huu majira ya saa 3:30 asubuhi katika eneo hilo mwanafunzi huyo alikutwa amejinyonga kwa kutumia kamba ya nailon akiwa chumbani kwake.
 
Kamanda Kashai alimtaja Marehemu kuwa ni Moses Iddi (28) Mnyamwezi ambapo baada ya tukio hilo alifariki dunia bila kupata msaada wowote
 
Amesema kuwa chanzo cha kujinyonga kwake ni kutokana na matokeo mabaya ya mtihani wake wa kumaliza kozi ya ualimu daraja A katika chuo hicho kilichopo Mkoani Tabora.
 
Kamanda kashai alisema kuwa awali kabla ya kujinyonga aliacha ujumbe wa maandishi uliosema kuwa kifo chake kisihusishwe na mtu yeyote.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo