Gari aina ya ya lsuzu lenye namba za usajili T 749 CCG baada ya kupata ajali eneo la Mindu mkoani Morogoro.
GARI aina ya Isuzu yenye namba za usajili
T749 CCG lililokuwa likisafirisha nyanya kutoka kijiji cha Mlali
kuelekea kwenye moja ya masoko ya mji wa Morogoro jana mchana lilipata
ajali na kupinduka eneo la Mindu jirani na bwawa la Mindu mkoani hapa.
Mashuhuda wa tukio hilo walidai kwamba
gari hilo lilipinduka baada ya kujaribu kumkwepa mwendesha bodaboda na
kwamba katika ajali hiyo hakuna mtu aliyepoteza maisha ingawa baadhi ya
wamiliki wa mizigo iliyokuwemo katika gari hilo walijeruhiwa.
'Unajua hivi vigari ni vyepesi sana hivyo
kikiyumba kidogo tu kinapinduka, wafanyabiashara kwa kawaida huwa
wanakaa juu ya matenga yao lakini kwenye tukio hili wamiliki wa matenga
hayo ya nyanya walikaa kwa dereva, sipati picha kama wangekaa juu ya
matenga yao kama ilivyozoeleka siku zote" alisema shuhuda huyo
aliyejitambulisha kwa jina la Johnson Joseph.
(Picha / Habari na Dustan Shekidele GPL, Morogoro