Mtu Mmoja Amefariki Dunia na Wengine Wawili Wamejeruhiwa Katika Ajali ya Barabarani Iliotokea Barabara ya Njombe -Lupembe Mkoani Njombe.
Taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoani Njombe Fulgency Ngonyani Imesema Ajali Hiyo Imetokea Agost Sita Mwaka Huu Ambapo Gari Lenye Namba za Usajili T 461 Aina ya Mitsubish Canter Mali ya Raymond Venant Mlowe Ikiendeshwa na Nemrand Kidolela Ilimgonga Mwendesha Baiskeli na Kusababisha na Majeruhi na Kifo Kwa Mtu Mmoja.
Amemtaja Mtu Aliefariki Kwenye Ajali Hiyo Kuwa ni Christopher Ngewe Mwenye Umri wa Miaka Sita na Kusema Kuwa Waliojeruhiwa Kwenye Ajali Hiyo ni Pamoja na Dereva wa Baiskeli Erick Ngewe na Franco Nduye Ambao Wote Wamelazwa Katika Hospitali ya Ikonda Wilayani Makete Kwa
Matibabu Zaidi.
Wakati Huo Huo Jeshi la Polisi Mkoani Njombe Linawashikilia Watu 18 Kwa Tuhuma Mbalimbali Akiwemo Mkazi Mmoja wa Mji Mwema Makambako Anaeshikiliwa Kwa Kukutwa na Pombe Haramu ya Gongo Lita Tano.
Kamanda Ngonyani Amesema Watuhumiwa Hao Wanatarajiwa Kufikishwa Mahakamani Wakati Wowote Kujibu Tuhuma Hizo.
NA GABRIEL KILAMLYA