Na Benedict Liwenga-MAELEZO.
WAZIRI wa Afrika Mashariki na
Mbunge wa Urambo Mashiriki, Mhe. Samuel Sitta amewaaasa vijana kutoa
maoni yao juu ya uundwaji wa Katiba mpya ambayo haijengi mifumno ya
serikli ya Udikteta, ubinafsi na ambayo haitaibebesha mzigo Serikali.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar
es Salaam na Mhe. Sitta wakati akifungua rasmi Baraza la Vijana la Taifa
la Katiba lililoandaliwa na Taasisi ya vijana ya Tanzania Youth
Coalition (TYC) kwa kushirikiana na Restless Development, UNFPA na ILO
lililojumuisha vijana 120 kutoka Wialaya 50 za mikoa yote Tanzania Bara
na Visiwani na ambao wanatoka katika mashirika mbalimbali, asasi,
jumuiya na vikundi mbalimbali vya vijana.
Waziri Sitta amewaasa vijana
kuwa TYC pamoja na vijana wengine nchini wanalojukumu kubwa la mapambano
dhidi ya kupinga ulafi katika mambo ya uongozi, udikteta pamoja na
ubinafsi kwani vinailetea mzigo serikali.
“Mtu ajue kuwa kutumia madaraka kwa manufaa yako mwenyewe ni mwiko”. Waziri Sitta alisema.
Waziri Sitta ameongeza kuwa
vijana nchini wanatakiwa wawe Wanaharakati katika kujali maadili mema na
kusimamia kwa dhati pamoja na kupigania haki na usawa nchini.
Aidha, kwa upande mwingine
Waziri Sitta amevishukuru vyombo vya habari kwa mchango wake mkubwa wa
kufanya kazi ya kuhabarisha umma na npia ameipongeza taasisi ya vijana
ya Tanzania Youth Coalition kwa kuandaa baraza hilo kwa vijana wenzao
kwani litawasaidia kutambiua mabo ya msingi yanayohitajika kuwepo katika
Katiba mpya ya nchi.
Waziri Sitta alisema kuwa
katika kutoa maoni juu ya Katiba mpya, vijana wanaweza kupata katiba
yenye manufaa mazuri au yenye athari kwa maisha yao, hivyo amewaasa
vijana wote watumie fursa wanazozipata kupitia baraza hilo
lililoandaliwa na TYC ili waweze kusikika katika mambo yanayohitajika
katika Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Taasisi ya vijana ya Tanzania
Youth Coalition ni moja ya taasisi iliyoundwa kwa malengo ya kuhakikisha
kuwa vijana wanashirki na kushirikishwa katika mchakato wa kuunda
katiba mpya ulioanza mwaka jana hapa nchini.