Picha ya pamoja
katikati ni Waziri wa Ushirkiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Samuel Sitta,
kushoto kwake ni Bwana Julius Toneshe na Meneja Mipango wa TYC Bi. Rahma Bajun.
Wa kwanza kutoka kulia kwake ni Kaimu
Mkurugenzi wa Taasisi ya Vijana ya Youth Coalition (TYC) Lenin Kazoba na Meneja
wa Restless Development.
Waziri wa Ushirikiano
wa Afrika Mashariki na Mbunge wa Urambo Mashariki, Mhe. Samuel Sitta
akiwahutubia vijana (hawapo pichani) waliohudhuria wakati wa ufunguzi wa Baraza
la Vijana la Taifa la Katiba lililofanyika leo 24/07/2013 jijini Dar es Salaam.
Bwana Julius Toneshe
aliyemwakilisha Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo akiongea wakati wa
ufunguzi wa Baraza la Vijana la Taifa la Katiba leo jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi wa
Taasisi ya Vijana ya Youth Coalition (TYC) Lenin Kazoba (kushoto) akitoa
maelezo mafupi kabla ya kumkaribisha rasmi Waziri wa Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Mhe. Samuel Sitta aliyekaa kulia wakati wa ufunguzi wa Baraza la
Vijana la Taifa la Katiba lililofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Meneja Mipango wa
Taasisi ya Vijana ya Youth Coalition (TYC) Bi. Rahma Bajun akiongea baada ya
kumkaribisha mgeni rasmi Mhe. Samuel Sitta kwa ajili ya kutoa hotuba yake na
kufanya ufunguzi rasmi wa Baraza la vijana la Taifa la Katiba leo 24/07/2013
jijini Dar es Salaam.
Mratibu wa Taasisi ya
Vijana ya Tanzania Youth Coalition Rebecca Gyum akiongea wakati wa ufunguzi wa
Baraza la Vijana la Taifa la Katiba lililofunguliwa rasmi na Waziri wa
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Samuel Sitta.
Baadhi ya washiriki
ambao ni vijana mbalimbali kutoka Wilaya 50 za mikoa yote Tanzania
wakimsikiliza kwa makini mgeni rasmi Mhe. Samuel Sitta (hayupo pichani) wakati
akitoa hotuba kwa vijana ha oleo jijini Dar es Salaam.PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-MAELEZO.