WAZEE WA ZAIDI YA MIAKA 70 WAFUNGA HARUSI MAKETE MKOANI NJOMBE


 Mzee Ezekia Sanga akiwa na mkewe Ester Mbilinyi baada ya kufunga ndoa
 mzee simon akifunga ndoa na mkewe Emeliana Mahenge
 kanisa walilotumia kufungia ndoa


Wananchi wa kijiji cha Maleutsi wilaya ya Makete mkoani Njombe hii leo wameshuhudia tukio la aina yake la vikongwe wawili kufunga pingu za maisha(harusi) tukio linalodaiwa kuwashangaza wengi na kuweka historia katika kijiji hicho

Harusi hiyo iliyofanyika katika kanisa katoliki Maleutsi limeshuhudiwa na umati mkubwa wa watu, ambapo wazee hao wanaokadiriwa kuwa na zaidi ya miaka 70 limehusisha ndoa mbili kati ya Ezekia Chaula na Ester Mbilinyi na nyingine ya Mzee Simon na Emeliana Mahenge wote wakazi wa kijiji hicho

Wakizungumzia tukio hilo wananchi wa kijiji hicho wamesema si kawaida kushuhudia tukio kama hilo na kuongeza kuwa hayo yaliyotokea yamekuwa fundisho kwa wengine hasa vijana ambao wanadhani suala la kufunga ndoa haliwezekani

“Ama kwa hakika hii ni ajabu kwa kweli maana wazee kama hawa wenye wajukuu na vitukuu kufunga harusi, maana wao wameshazeeka na hawana haja hiyo tena na hata wasingefanya hivyo hakuna wa kuwauliza maana umri umekwenda, kwa kweli hii ni ajabu lazima sisi kama vijana tujifunze” alisema Eliza sanga

Tukio hilo linadaiwa kuweka historia kubwa katika kijiji hicho na wilaya ya Makete kwa ujumla


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo