
KWA
SABABU:- Sisi wananchi hatujashirikishwa kupitia mjadala wa Bunge
kuhusu kodi hii kwani Waziri wa fedha hakusoma hiki kipengele wakati wa
hotuba yake na tulikosa taarifa mpaka baada ya kupitishwa kwa sheria ya
kodi hii.
KWA SABABU:-
Kodi hii inamkandamiza mtanzania wa hali ya kawaida na wa hali ya chini
ambao ni 67% ya wananchi wanaoishi chini ya kipato cha dola 1.25 (shs
2,000) kwa siku. Takwimu zinaonyesha kuwa kati wa wamiliki wa laini za
simu milioni 22, milioni 8 wanatumia chini ya shilingi 1,000 kwa mwezi.
Kuwaongezea mzigo wananchi hawa kwa kiwango ambacho tayari wanashindwa
kumudu ni kuwanyima kabisa fursa ya kutumia huduma hii muhimu.
KWA SABABU:- Kodi hii
haifuati misingi ya kulipa kwa kadri ya matumizi na ni kodi kandamizi
inayowatoza wamiliki wa laini ya simu wote kiasi kimoja bila kuzingatia
kiwango cha matumizi. Hii inamkandamiza mwananchi wa hali ya chini kwa
kumlazimisha kulipa kiwango kikubwa cha kodi kulingana na mapato yake.
Tukichukulia mfano wa mtu anayetumia shilingi laki tano kwa mwezi kama
muda wa maongezi na yule anayetumia shilingi elfu tano - na
tukilinganisha uwiano wa malipo haya na matumizi yao – basi yule
anayetumia shilingi laki tano analipa 0.2% ya matumizi yake, ila yule
anayetumia shilingi elfu tano anatozwa 20% ya matumizi yake.
KUTOKA KWA MDAU BOFYA LINK HIYO HAPO CHINI KUSOMA ZAIDI.
Kaka tafadhali ninaomba utuwekee patition
hii kwenye blog yako ili watanzania washiriki katika kuweka sahihi
katika kupinga zuio la ongezeko la kodi katika line za simu. Asante