WANANCHI WA KIJIJI CHA ILOVELO KATA YA LUPALILO WILAYANI MAKETE WAKERWA NA WATENDAJI WAO

 
Wananchi wa Lupalilo wakimsikiliza mbunge wao Dr Bililith Mahenge akiwahutubia
Mbunge wa jimbo wa Makete na Naibu waziri wa maji Dr Binilith Mahenge akiwahutubia wananchi wa kata ya Lupalilo.
 

Licha ya Serikali Kuwaagiza Watendaji wa Vijiji na Kata Kusoma Hesabu za Mapato na Matumizi Kila Baada ya Miezi Mitatu, Bado Agizo Hilo Linaonekana Kutotekelezwa na Baadhi ya Watendaji Hao Katika Mikoa Mbalimbali Ukiwemo Mkoa wa Njombe.

Hali Hiyo Imejitiokeza Wilayani Makete Baada ya Wananchi wa Kijiji cha  Ilovelo Kata ya Lupalilo Kulalamika Kutosomewa Taatifa ya Hesabu na Mapato na Matumizi Kwa Kipindi cha Takribani Miaka Mitatu Hadi Sasa.

Wakiongea Kwenye Mkutano wa Hadhara Mbele ya Naibu Waziri wa Maji na Mbunge wa Makete Dk. Binilith Mahenge Wamesema Wamekuwa Wakichangia Fedha Kwa Ajili ya
Utekelezaji wa Miradi Mbalimbali ya Maendeleo Kijijini Humo Ikiwemo Ujenzi wa Zahanati Lakini Hadi Hivi Sasa Hakuna Jitihada Zozote Zinazoonesha Kuanza Kwa Ujenzi Huo na Hakuna Taarifa Yeyote Inayoelezea Kutoanza Kwa Utekelezaji wa Miradi Hiyo.

Wamesema Kutokana na Uongozi wa Kijiji Hicho Kuwa Mbovu  Hawako Tayari Kuendelea Kuchangia Michango Kwa Ajili ya Miradi Yoyote Hadi Hapo Uongozi wa Kijiji Utakapobadilishwa .

Kufuatia Malalamiko ya Wananchi Hao Naibu Waziri Huyo wa Maji Dk. Mahenge Amemuagiza Diwani wa Kata Hiyo Pamoja na Katibu Tarafa wa Lupalilo Kwa Kushirikiana na Mkurugenzi Kuandaa Uchaguzi Katika Kijiji Kwa Ajili ya Kuwapata Viongozi Watakao Simamia Shughuli za Maendeleo Kwa Maslahi ya Wananchi.

Na James Festo


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo