SERIKALI YAIFUNGA MIGODI MINNE MERERANI

 Name:  IMG_0456.jpg
Views: 0
Size:  1.08 MB
Kufuatia kupigwa risasi kwa mfanyakazi wa Tanzanite one William Onesmo Mushi (pichani) na kufariki papo hapo serikali kupitia wizara ya nishati na madini imefunga migodi minne inayozunguka eneo hilo kwa muda usiojulikana ili kupisha uchunguzi wa kina kufuatia tukio hilo.

Kamishna Msaidizi wa madini kanda ya kaskazini Benjamin Mchwampaka alitaja migodi iliyofungwa kuwa ni inayomilikiwa na Joseph Mwakipesile maarufu kwa jina la Chusa,Abdulhakimu Mula,Maning'oo na Jackson Saimon.


Aidha Jeshi la polisi mkoa wa Manyara linamshikilia Chusa kwa mahojiano kuhusiana na tuhuma za kudaiwa kuhusikana kifo cha Mushi usiku wa kuamkia Julai 20 mwaka huu.


Uchunguzi wa madaktari wa mwili wa marehemu umebaini kuwa maremu aliuwawa kwa kupigwa risasi mbili kifuani upande wa kushoto zilizomsababishia kifo cha papo hapo.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo