WAKAZI wa kijiji kimoja Kaunti ya Murang’a ambapo inashukiwa punda alibakwa hadi kufa walifanya maombi mnamo Jumatano hii ili kujitakasa.
Wakiongozwa
na wahubiri kutoka makanisa kadhaa kutoka sehemu hiyo, wakazi wa kijiji
cha Nyati, Lokesheni ya Kamahuha katika eneo bunge la Maragua
walikashifu kitendo hicho na kumwomba Mungu msamaha.
Mhubiri
Joseph Kamande wa dhehebu la Akorino eneo la Kamahuha alilinganisha
kitendo hicho na miji ya Sodoma na Gomorrah katika Kitabu cha Mwanzo
kwenye Biblia.
“Hili ni
jambo la kushangaza na tunafaa kuomba Mungu atusamehe, hatutaki kijiji
chetu kiwe kama Sodoma na Gomorah,” alisema Mhubiri Kamande akiwahutubia
wakazi katika uwanja wa Nyayo ambapo kulitokea kisa hicho.
Inadaiwa wanamme ambao idadi yao haijulikani walimchafua punda huyo wa kiume hadi akafa wakati wa usiku.
Mnyama huyo
wa thamani ya Sh15,000 aliyekuwa anamilikiwa na Bw Peter Murigi
alipatikana akiwa amefungiliwa chini ya mti wa mwembe akiwa amekufa
katika uwanja wa Nyayo huku mipira 10 ya kondomu ambayo ilikuwa
imetumiwa ikiwa imetapakaa mahali hapo.
Kesha
Cha kushangaza ni kuwa kisa hicho kilitokea mita chache tu kutoka kwa kanisa moja ambapo maombi ya kesha yalikuwa yanafanyika.
“Hatujui ni
shetani mgani amewashika wanamme wetu na sote tuko hatarini ya
kunajisiwa na waliochafua punda huyo,” alisema Bi Esther Muthoni huku
majonzi ya huzuni yakimtoka.
“Hizi ni siku za mwisho ambazo zilitabiriwa na manabii wa Biblia na tunaomba Mungu atusaidie,” alilia Bi Muthoni.
Na SAMUEL KARANJA