VIJANA mkoani Iringa wametakiwa kushiriki katika afya
ya uzazi kwa vijana ili kuzijua na kuzitambua haki za afya ya uzazi kwa vijana
na kutambua mahitaji yao muhimu.
Akizungumza leo,Ofisa utetezi na sera wa
mradi wa haki ya afya ya uzazi kwa vijana Meshack Mollel alisema kuwa vijana
wanatakiwa kushiriki na kupata elimu ya afya ya uzazi ili kujitambua na kujua
haki zao na kuunda sera zinazowahusu.
Mollel alisema kuwa mradi huu unatekelezwa katika
manispaa tatu ikiwamo IRinga , Ilala na
Kinondoni ili kutoa elimu ya afya ya uzazi kwa vijana kwa kushirikiana na shirika la afya na tiba AMREF chini ya ufadhili wa shirika maendeleo
la nchini swedeni(SIDA).
“Tamasha hili la vijana lenye kauli mbiu inayosema “hamasisha
ushiriki wa vijana ili kutambua mahitaji muhimu katika afya ya uzazi”pia tukiwa
na lengo la kutoa elimu na kuzijua haki
za afya ya uzazi kwa vijana na kuwapa fursa ya kuunda sera zinazo wahusu
vijana”alisema Mollel.
Kwa upande wake naibu meya wa manispaa ya Iringa Gervas
Ndaki ambaye alikuwa mgeni rasmi alisema kuwa anafurahi kuwaona vijana
wamejitokeza kwa wingi hivyo anaimani hata katiba mpya ya sasa itakuwa na maoni
na sera zinazo muhusu kijana.
“dhana hii ya michezo ni dhana nzuri ya kuwakutanisha
vijana kwa sababu kwanza michezo inapendwa na vijana
wengi na inajenga afya zao na kuwa fanya
waondokane na makundi yasiyofaa kutokana na vijana kuwa na changamoto
nyingi”alisema Ndaki.