Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi
akikagua guard ya wahitimu wa Jeshi la Polisi na Uhamiaji kabla ya kuyafunga
mafunzo ya wahitimu hao ya awali yaliyofanyika katika Chuo Cha Polisi
(CCP) mjini Moshi jana .Wahitimu 3,092 wakiwemo askari wa Uhamiaji 51
walimaliza mafunzo hayo jana. Dk. Nchimbi katika hotuba yake aliwataka
wahitimu hao kufanya kazi kwa uadilifu katika vituo mbalimbali vya kazi
watakavyopangiwa nchini.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (kushoto) akisalimiana na Katibu
Mkuu wa wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil pamoja na viongozi mbalimbali
wa wizara na maofisa wa Jeshi la Polisi wakati alipokuwa anawasili katika
viwanja vya Chuo Cha Polisi (CCP), mjini Moshi kwa ajili ya kufunga
mafunzo ya awali ya Polisi na Uhamiaji.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi
akifungua bomba la maji la kisima baada ya kukizindua katika Chuo Cha
Polisi (CCP) mjini Moshi. Dk Nchimbi pia alitembelea miradi mbalimbali
iliyopo ndani ya chuo hicho kabla ya kufunga mafunzo ya awali ya Polisi
na Uhamiaji namba 1/2012/2013.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (kulia) akimkabidhi zawadi mmoja wa wahitimu waliofanya
vizuri katika masomo yao wakati wa mafunzo ya awali ya Polisi na Uhamiaji
yaliyofanyika katika Chuo Cha Polisi (CCP) mjini Moshi leo. Wahitimu
3,092 wakiwemo askari wa Uhamiaji 51 walimaliza mafunzo hayo Jana. Dk.
Nchimbi katika hotuba yake aliwataka wahitimu hao kufanya kazi kwa uadilifu
katika vituo mbalimbali vya kazi watakavyopangiwa nchini.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi
akitoa hotuba yake kwa wahitimu wa mafunzo ya awali ya Polisi na Uhamiaji
(hawapo pichani) kabla ya kuyafunga mafunzo hayo katika Uwanja wa Chuo
Cha Polisi (CCP) mjini Moshi. Wahitimu 3,092 wakiwemo askari wa Uhamiaji
51 walimaliza mafunzo hayo jana. Dk. Nchimbi katika hotuba yake aliwataka
wahitimu hao kufanya kazi kwa uadilifu katika vituo mbalimbali vya kazi
watakavyopangiwa nchini.
PICHA ZOTE
NA FELIX MWAGARA
KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI WIZARA
YA MAMBO YA NDANI YA NCHI.