Kutokana na vitendo vya ubakaji kushamiri katika mkoa wa Iringa, Kamanda wa jeshi la polisi RAMADHANI MUNGI amekemea vikali vitendo
hivyo na kusema kuwa ni makosa dhidi ya Binadamu.
Akizungumza,Kamanda
Mungi amesema kuwa mtu yoyote anayefanya mapenzi na msichana au binti
chini ya umri wa miaka 18 hata kama atakuwa amekubali kwa hiari yake
bado atahesabiwa kuwa mbakaji.
Mungi
amesema kuwa vitendo hivyo vinasababishwa na matatizo ya kisaikolojia
hivyo watalamu wa saikolojia wanapaswa kulishugulikia suala hilo ili
kusaidia kupunguza matukio kama hayo.
Aidha
ameongeza kwa kusema kuwa kutokana na wananchi wengi kulalamika juu ya
kuachiwa huru kwa watuhumiwa wenye makosa ya ubakaji, amesema kuwa ni
haki yao kupewa dhamana kwa mujibu wa sheria na sio kwamba polisi
wanafanya makusudi.