MWANAMKE AUAWA ANYOFOLEWA VIUNGO VYA MWILI WAKE

Mkazi wa kijiji cha Mwalisi kata ya Ngana wilayani Kyela Mkoani Mbeya Enita Kalota (23)amekutwa amekufa katika maeneo ya Kitongoji cha Kandete kijiji cha Ngana   huku akiwa amenyofolewa baadhi ya viungo katika mwili wake,
 
Akizungumza na Ripota wetu ofisini kwake kaimu ofisa mtendaji wa kata hiyo ya Ngana Joseph Mapunda alidai kuwa ofisi yake ilipata taarifa ya kuwapo mtu aliyeuawa katika kijiji hicho cha Ngana mnamo majira ya saa 3 asubuhi jana na baada ya hapo walitoa taarifa kituo kidogo cha Polisi cha Kasumulu,
 
Alisema msichana huyo alikuwa anaishi Boda ya Kasumulu baada ya kumaliza shule darasa la saba miaka ya hivi karibuni  katika shule ya msingi  Mwalisi alianza kufanya shughuri za kuuza vinywaji kwenye baa na kuwa jana walishangazwa baada ya kuuona mwili wa msichana huyo akiwa amefia katika kijiji cha Ngana,
 
Mapunda alifafanua kuwa mbali na kuwepo kwa tukio hilo hakufanikiwa kuuona mwili huo na kuwa anasubiri kuletewa ripoti kutoka kwa afisa mtendaji wa kijiji ili aziweke katika kumbukumbu ambapo wakazi wa eneo hilo waliouona mwili huo wanadai kuwa  walivyoutizama mwili wa mwanamke  huyo walikuta baadhi ya viungo vyake vikiwa havipo kama sikio, ngozi ya kisogoni vikiwa imeondolewa huku kukikwa na tetesi kuwa hata sehemu zake za siri nazo zimeondolewa,
 
Kwa upande  wake mwenyekiti wa kijiji cha Ngana Stanley Shimwela alisema kuwa tukio hilo limewashitua sana wananchi wa kijiji hicho ukichukulia hilo ni tukio la tatu kwa mwaka huu wa 2013 ambapo vifo vyote uhusishwa na imani za kishirikina baada ya maiti zote zilizouawa kunyofolewa baadhi ya viungo vya mwili,
 
Mganga wa zamu katika hospitali ya wilaya Kyela aliyeufanyia uchunguzi mwili huo Dkt,Nsubiri Mwansule alisema kuwa baada ya wao kuufanyia uchunguzi mwili huo walibaini msichana huyo kupigwa na kitu chenye ncha kali eneo la kisogoni kichwani kilichopelekea maumivu makali na kupelekea kifo cha mwanamke huyo,
 
Alisema kuwa hawezi kusema lolote juu ya kutokuwepo kwa baadhi ya viungo ambavyo havipo katika mwili wa marehemu kwa madai kuwa yeye si mmsemaji wa hospitali hiyo,
 
Kaimu mganga mkuu wa hospitali ya wilaya Dkt Apaisaria Rumisha alipotafutwa ili kulitolea ufafanuzi jambo hilo hakuweza kupatikana kwa madai kuwa yupo katika ofisi za halmashauri ya wilaya kwenye kikao.
 
Jeshi la polisi Wilayani hapa waliruhusu familia ya marehemu kuendelea na taratibu za mazishi baada ya mwili huo kufanyiwa uchunguzi huku wao wakiendelea na uchunguzi wa kuwabaini wahusika wa tukio hilo,
 
Wananchi kwa upande wao wameiomba kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya ya Kyela kufanya juhudi za haraka za kuhakikisha wanakemea vitendo hivyo ili kuweza kupunguza vitendo hivyo vya mauaji vinavyotokea kwa imani za kishirikina vinavyoipa sifa mbaya Wilaya ya Kyela,
 
Wamesema kuwa  Mkoa wa Mbeya  unaongoza kuwa na makanisa mengi ukilinganisha na mikoa mingine ambapo kila kata kuna zaidi ya makanisa matano lakini ndiyo Mkoa wa kwanza kuwa na matukio mengi yanayohusishwa na imani za kishirikina na biashara haramu za kuuza viungo vya binadam.

Na Ibrahim Yassin


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo