MGAMBO 30 WANUSURIKA KIFO BAADA YA KUPIGWA NA WAFANYABIASHARA KINONDONI

Zaidi ya mgambo wa manispaa ya Kinondoni 30 pamoja na polisi jamii wa kata ya Makumbusho wapatao 32 wamenusurika kufa kwa kipigo na kulazimika kukimbia baada ya kushambuliwa na wafanyabiashara wa soko la Mwananyamala wakati wakifanya zoezi la kuwaondoa wafanyabiashara hao katika maeneo yasiyo rasmi pembezoni mwa soko hilo.
 
Mwandishi wetu amefika katika hospitali ya Mwananyamala na kukuta mgambo hao wakiwa na majeraha makubwa vichwani, huku wengine wakiwa katika chumba maalum kwa ajili ya kushonwa majeraha yaliyotokana na kipigo kikali toka kwa wafanyabiashara hao ambao kwa kiasi kikubwa inadaiwa wamekiuka sheria kwa kufanya biashara katika maeneo yasiyo rasmi.
 
Akizungumza na waandsihi wa habari, afisa mtendaji kata ya Makumbusho Bibi Husna Nondo amesema operesheni hiyo imeandaliwa ili kuondoa wafanyabiashara hao wasio rasmi katika soko hilo kutokana na kuwa karibu na barabara pamoja na shule za Mwananyamala B. na  shule ya Minazini na kuwafanya wanafunzi kushindwa kusoma kutokana na kelele  hali iliyochangia kuwa na matokeo mabaya katika mitihani iliyopita. 
 
Mkurugenzi wa manispaa ya Kinondoni bwana Mussa Natty amewataadharisha baadhi ya wafanyabiashara wanaojichukulia hatua mikononi na kuwapiga mgambo wa manispaa kinyume cha sheria ambapo amesema katika kukabiliana na matukio ya namna hiyo yanayoendelea kujitokeza manispaa inaangalia uwezekano wa kutumia jeshi la polisi katika operesheni mazingira ili kuweka mji safi.
 
CHANZO: ITV


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo