MWANAMKE AVULIWA NGUO AKIHISIWA KUIBA SH. 1,100

Embu
Mji wa Embu.

Na CHARLES WANYORO
KIZAAZAA kilizuka katika soko la Kimangaru wilayani Embu Magharibi Alhamisi mwanamke wa miaka 30 alipovuliwa nguo na wakazi kwa madai ya kumwibia mwanaume aliyekuwa anakunywa naye pombe.
Mwanamke huyo ambaye ni mama wa watoto wawili, alidaiwa kuiba Sh1,100 ambazo mwanaume huyo alikuwa ameziweka juu mezani na kuzificha katika nguo zake za ndani.
 
Mwanamume huyo anadaiwa kumsihi mwanamke huyo amrejeshee pesa hizo lakini akakataa na kusisitiza kwamba hakuwa amezichukua.

Kulingana na Mike Murithi, mwendeshaji boda boda ambaye alishuhudia kisa hicho, mwanaume huyo aliungana na wanaume wengine na kumvua nguo zote wakitafuta pesa hizo.

“Tulipata walevi wengi wakimvua nguo. Mwanzo walizisaka kwenye jaketi, kisha wakamvua blausi. Walipata pesa hizo baada ya kumvua long'i,” alisema.

Baada ya kupata pesa hizo, wanaume hao walimfukuza mwanamke huyo na wakaendelea kujiburudisha.

"Wawili hao walikutana tu kwenye baa. Mwanamke huyo huwa anajiburudisha na wanaume kwenye mabaa mbalimbali mjini. Wanaume hao hata hivyo hawakumpiga," akasema Bw Murithi.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo