Picha juu na chini Diwani
mteule wa kata ya Themi Arusha Ndugu Melance Kinabo(KABURU) kupitia
CHADEMA akizungumza na wakina mama ambao ni wakulima wa mbogamboga waliomuita kwa simu
kumuomba msaada baada ya mwenyekiti wa Mtaa wa Themi Magharibi Mzee
Dions Msele - CCM kukataza matumizi ya mfereji wa kumwagia maji ktk
mashamba ya kina mama wa mtaa husika bila sababu za msingi.
----
Diwani
mteule wa kata ya Themi Arusha Ndugu Melance Kinabo(KABURU) kupitia
CHADEMA ameanza kazi zake rasmi kama diwani hili hali bado hajaapishwa.Leo
tarehe 29 - June 2013 mishale ya saa tisa alasiri Diwani wa Themi Ndugu
Kaburu aliwasili mtaa wa Fire maeneo ya magorofa ya polisi kusikiliza
kilio cha kina mama ambao ni wakulima wa mbogamboga waliomuita kwa simu
kumuomba msaada baada ya mwenyekiti wa Mtaa wa Themi Magharibi Mzee
Dions Msele - CCM kukataza matumizi ya mfereji wa kumwagia maji ktk
mashamba ya kina mama wa mtaa husika bila sababu za msingi.
Diwani huyu wa Themi kupitia Chadema aliwahoji kina mama husika na kugundua kuwa Mwenyikiti wa mtaa hakuwa na sababu za msingi za kuwazuiya kina mama hao kuendelea na kilimo cha umwagiliaji kupitia mfereji husika.
Diwani huyu mteule akuchukua hatua ya kuhoji tatizo husika kwa mtendaji wa kata ya Themi na kugundua kuwa kina mama hawa wa Themi Magharibi wananyanyaswa na mwenyekiti wa mtaa Dions Msele - CCM na ndipo akatoa amri kuwa mfereji huo ufunguliwe na kina mama waendelee na kilimo cha mboga bila kusumbuliwa na pia ametoa ahadi ya kusimamia utengenezaji wa kalavat kwenye mfereji husika kuepusha ajali kwa watoto wa polisi wanaoishi maeneo ya Themi Magharibi karibu na chanzo cha mfereji huo ulioleta utata.