
Mlinda mlango mpya aliyesajiliwa na mabingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom
Tanzania bara Deogratius Munishi 'Dida' pamoja mlinzi wa kati aliyekua
akiichezea timu ya Mtibwa Sugar msimu uliopita Rajab Zahir leo wameanza
rasmi mazoezi na timu yao ya Young Africans Sports Club kwa ajili ya
msimu mpya 2013/2014.
Deogratius Munishi 'Dida' ameungana na wachezaji wengine wawili
mshambuliaji Shaban Kondo aliyekua akicheza soka nchini Msumbiji pamoja
na mlinzi wa kati Rajab Zahir aliyerejea kutoka nchini Afrika Kusini
alipokuwa akifanya majaribio katika timu mbili za Ligi Kuu nchini humo.
Mapema
jana katika siku ya kwanza ya mazoezi kiungo mshambuliiaji Mrisho
Khalfani Ngasa alifanya mazoezi asubuhi chini ya kocha mholanzi Ernest
Brandts kabla ya kocha huyo kuwapa nafasi wachezaji wote wa timu ya
Taifa kujiunga na timu leo kwa ajili ya maandalizi ya mchezo dhidi ya
Uganda julai 13 Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Mpaka sasa klabu ya Yanga imefanikiwa kusajili wachezaji watano ambao ni:
1. Deogratius Munishi 'Dida' - Huru (Azam)
2. Rajab Zahir - Huru (Mtibwa)
3. Mrisho Ngassa - Huru (Azam)
4. Shaban Kondo - Huru
5. Realitus Lusajo - Machava FC
Kocha
Brandts amefurahia kuongezeka kwa wachezaji hao kwani amesema atapata
fursa ya kukaa nao na kucheza michezo ya kirafiki kanda ya ziwa hali
itakayopelekea kupata nafasi ya nzuri kukiandaa kikosi na msimu mpya wa
2013/2014.
Yanga itaendelea na mazoezi kesho asubuhi katika uwanja
wa shule ya sekondari Loyola ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya ziara
yake kanda ziwa inayotazamiwa kuanza mwishoni mwa wiki jijini Mwanza.
Wachezaji
wote wameendelea na mazoezi leo asubuhi isipokua wachezaji waliojiunga
na kambi ya timu ya Taifa kwa ajili ya mchezo dhidi ya Uganda