CHADEMA YAFURAHIA USHINDI WA KISHINDO ARUSHA


Matokeao  ya uchaguzi katika kata nne za jiji la Arusha ambazo zote zimechukuliwa na Chama cha demokrasia na maendeleo Chadema yamepokelewa kwa shangwe na furaha kubwa na viongozi na  wanachama wa chama hicho.
 
Miongoni mwa viongozi waliozungumzia matokeo hayo ni pamoja na mbunge wa jimbo la Arusha Mh Godbless Lema ambaye amesema matokea hayo pamoja na kuwapa wananchi wa Arusha nafasi kubwa  ya kuleta mabadiliko yametoa mwelekeo mpya wa Chama hicho katika harakati zake za kuongoza nchi   uchaguzi ujao.
 
Katika uchaguzi huo uliofanyika  kwa  amani ukihusisha kata za kaloleni themi , kimandolu, na elerai pamoja na kufanyika kwa amani na utulivu mkubwa huku ulinzi ukiwa umeimarisha kila kona katika vituo vya uchaguzi, vituo vya kuhesabu kura na kona mbalimbali za jiji la Arusha changamoto kubwa ilikuwa ni idadi ndogo ya watu waliojitokeza kupiga kura ikilinganishwa na Waliojiandisha.
 
Baada ya kutangazwa kwa matokeo hayo ya madiwani wapya wa kata zote nne ikiwemo ya Kaloleni  inayoongozwa na Bw. Kessy Emmanuel  Elerai ambayo kwa sasa inaongozwa na mhandishi  Jeremia  Mpinga, Kimandolu inayoongowa na Rayson Ngowi na Themi inayoongozwa na kinabo Meladi  wanachama wa Chadema wengi wao wakiwa ni vijana walilipuka kwa nderemo na vifijo wakishangilia  ushindi huo.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo