WAZIRI DK MGIMWA AWASILISHA BAJETI YA SERIKALI 2013/2014 BUNGENI DODOMA LEO

 
 Waziri wa Fedha Dk William Agustao Mgimwa
Waziri wa Fedha Dokta William Mgimwa amewasilisha Makadirio ya Bajeti kuu ya Serikali inayotarajia kutumia Shilingi Trilioni 18.2 kwa mwaka wa fedha 2013/2014 sawa na ongezeko la asilimia 17 ya bajeti ya mwaka 2012/2013.

Akiwasilisha bajeti hiyo Bungeni mjini Dodoma Dokta Mgimwa amesema vipaumbele vipo katika Miundombinu, Kilimo, Viwanda, Kuimarisha Utalii pamoja na Huduma za Jamii

Waziri huyo pia ameelezea Misingi ya Bajeti hiyo ambayo ni kuendelea kuimarisha na kudumisha amani na usalama, kudumisha viashiria vya uchumi, na kuimarisha sera za fedha ili ziendane na sera za bajeti husika.

Aidha amezitaja Bidhaa ambazo bei zake zitabaki vile vile na zingine zikiongezeka bei akisisitiza ushuru wa maji yanayozalishwa viwandani hautoongezwa

Akiwasilisha Taarifa ya Kamati ya Bunge ya Bajeti, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mheshimiwa Andrew Chenge amesema miradi ya maendeleo haitengiwi fedha za kutosha hali inayosababisha kutotekelezwa kwa wakati.

Serikali itatumia shilingi Trilioni 5.67 (31.9%) ya Bajeti yote kutekeleza mipango ya maendeleo ambapo shilingi Trilioni 2.68 ni kutokana na mapato ya ndani.

Malengo ya Bajeti ya mwaka 2013/14 ni pamoja na pato la taifa kukua kwa asilimia 7.0 mwaka 2013 2014 na asilimia 7.2 mwaka 2013, kuendelea kudhibiti kasi ya upandaji bei ambapo mfumo wa bei unatarajiwa kushuka zaidi ya asilimia 6.0, kuongezeka kwa mapato ya ndani kwa asilimia 20.2 mwaka 2013 /2014 pamoja na kuwa na akiba ya fedha za kigeni itakayoweza kukidhi mahitaji kwa kipindi kisichopungua miezi 4 kwa mwaka 2013.2014.

Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Mahusiano na Uratibu Stephen Wasira ameelezea mwenendo wa uchumi kwa Taifa.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo