Kampala, Uganda. Moto mkubwa umeweka
baada ya ajali mbaya ya barabarani kutokea na kuhusisha lori la mafuta.
Moto huo umewauwa watu 29 mjini kampala Uganda, hivi punde.
Pia watu wengine 30 wamejeruhiwa vibaya kufuatia tukio hilo.
Maofisa wa polisi wanasema kati ya waliofariki dunia ni raia
waliokuwa wanakimbilia kwenye eneo ambako ajali hiyo imetokea kwa ajili
ya kuteka mafuta yaliokuwa yakivuja kutoka kwwenye lori hilo.
Maofisa wa serikali wa hivi sasa wako kwenye harakati za kutambua
mili ya watu waliofariki dunia kwenye eneo la ajali baada ya watu wengi
kuungua vibaya.
Idara ya polisi imesema watu waliofariki dunia waliteketea kiasi cha
kutotambulika na itabidi watumie utaalamu wa vinasaba au DNA kutambua
miili ya waliokufa.