WATATU WAFIKISHWA MAHAKAMANI MBEYA KWA TUHUMA ZA MAUAJI YA KUKUSUDIA YA MWENYEKITI WA SACCOS

Jailo Rashid (30), Niza Hamis (24) na Medi Keya(33) ambao kwa pamoja wanadhaniwa kumuua kwa makusudi, Ambrose Shayo(45) aliyekuwa ni Mwenyekiti wa Umoja wa Saccos Taifa na Tazara Saccos ya Jijini Mbeya.
Hili ndilo eneo alilouawa mwenyekiti huyo wa saccos

WATU watatu wamefikishwa mahakamani wakituhumiwa kutenda kosa la kumuua kwa kukusudia aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha kuweka na Kukopa (Saccoss), Mbeya

Akisoma mashtaka hayo, Mwendesha Mashtaka wa Serikali Hebel Kihaka mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Mbeya Venance Mlingi alidai Watuhumiwa hao kwa pamoja walitenda kosa la mauaji kwa makusudi kinyume cha Sheria ya Makosa ya Jinai kifungu cha 196 sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.

Aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Jailo Rashid (30), Niza Hamis (24) na Medi Keya(33) ambao kwa pamoja walimuua kwa makusudi, Ambrose Shayo(45) aliyekuwa ni Mwenyekiti wa Umoja wa Saccos Taifa na Tazara Saccos ya Jijini Mbeya.
 
Alisema watuhumiwa hao kwa pamoja walitenda kosa hilo  April 20, Mwaka huu majira ya saa 3 usiku katika Kijiji cha Itagano Kawatere Jijini Mbeya ambapo Marehemu alivamiwa na watu hao kisha kumuua.

  
Kwa upande wake Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo Venance Mlingi alisema Kwa mujibu wa Sheria watuhumiwa hawaruhusiwi kujibu chochote kutokana na Mahakama yake kutokuwa na uwezo wa kusikiliza Shauri la Mauaji.
  
Aliongeza kuwa Shauri hilo limeletwa kwa ajili ya hatua za awali ambapo baada ya upelelezi kukamilika litapelekwa Mahakama kuu kwa ajili ya taratibu za kusikiliza, pia aliahirisha kesi hiyo hadi Julai 3, Mwaka huu itakapotajwa tena.

Na Mbeya yetu


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo