Baadhi ya wasomi na wananchi mkoani Iringa wamepongeza
rasimu ya katiba iliyotangwa jana Jijni Dar es Salaam na kufafanua kuwa imefuta makosa
ya awali yalikuwa kwenye muundo wa Tume ya mabadiriko ya katiba mpya.
Akizungumza ofisini kwake mjini hapa Mkuu wa Kitivu cha
Sanaa na Sayansi Jamii wa Chuo Kikuu cha Tumain Profesa Seth Nyagava alisema
rasimu hiyo inatoa matumaini makubwa kwa Tanzania ijayo kwa kuwa imebabu mbao
yote ya msingi yaliyokuwa yakidiwa na wananchi.
Alitaja mambo hayo kuwa ni kupunguza madaraka ya rasi,muundo
wa muungano kuw ana serikali tatu,kuwa na ukomo wa kipoindi cha ubunge na
muundo wa baraz ala mawaziri.
Alisema hatua ya mawaziri kuthibitishwa na bunge ni jambo
jema kwa kuwa litawezesha wananchi kujenga imani na viongozi wao na kuondoa
dhana iliyojengeka kuwa viongozi wanachaguana kwa vigezo vya urafiki.
“Mimi sijasoma rasimu yenyewe kwa undani,lakini kwa haya
niliyoyasikia nimefurahisha sana nayo,lipo suala la kupungua kwa madaraka ya rais,muundao wa muungano kuwa
na serikali tatu na mawaziri kuthibitishwa na Bunge, masuala haya ni muhimu
katia usatwi na Ujezni wa Taifa hili,”alisema Profesa Nyagava na
kuongeza:
“ikiwa mawaziri watathibitishwa na Bunge hali hiyo itaondoa dhana
iliyojengeka kuwa rais aliyoko mdarakani
kuchagua watu kwa kutumia vigezo vya urafiki kwa kuwa wahusika watahojiwa kwa kina
na kabla ya kuthibitishwa kushika nyazifa zao”.
Profesa Nyagava ambaye alikuwa bado anaipitia rasimu hiyo
alisema kazi iliyofanywa na Tume ya mabadiliko ya katiba chini ya Jaji Mstaafu
Joseph Warioba inapasw akupongez wana kuongeza kuwa imefuta mawazo na hofu
ilikuwa umejengeka wakati wa uundwaji wa baraza kwa madai ya lingeitenda haki.
Kwa upande wake Mhadhiri wa Chuo cha Tumaini ambaye pia ni
Mkuu wa Kitivo cha sheria ,Wakili Renatus Mgongo alipongeza tume kuja na rasimu
bora inayozingatia haki za bindamu,miiko ya viongozi wa umma,na haki za kupata
habari na kusambaza inayotoa uhuru kwa vyombo vya habari kufanya kazi yake.
Alitaja jambo jingine alilodai ni muhumu katika kujenga
usatiwa wakitaifa kuw ani kutajwa kwa miiko
ya viongozi wa umma katika rasimu ya katiba hiyo akidai itasaidia
kuonyesha dira ya taifa la Tanzania.
“Baada ya kufa kwa zimio la Arusha ambalo lilikuwa na miiko
taifa lilibaki bila miiko kwa viongozi wake ,lakini rasimu hii imekuja na
majibu ya matakwa ya wananchi kwa kuweka kipengele kinachoelezea utii wa miiko
ya viongozi”alisema Mgongo.
Mgongo aliwataka watanzania kuisoma katiba hiyo na kabla ya
kuanza kutoa maoni yao ili waweze kuelewa vema rasimu ya katiba hiyo kabla ya
kwenda kuijadili.
Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabishara wa Viwanda
na wakulima (TCCIA)Tawi la Iringa Lucas
Mwakapungu alisema rasimu ya katiba imejibu madai yaliyomengi ya wanachi.
“Uwepo wa serikali tatu ni hitaji muhumu katrika muundo wa muungano na hii itasaidia hata suala zima la mgawanyo wa madaraka na
kurahisha utendaji kazi kwa kila sehemu ya muungano”alisema Mwakapungu