skip to main |
skip to sidebar
DKT KAWAMBWA NA MULUGO WAMESHINDWA KUONGOZA WIZARA YA ELIMU - SUZAN LYIMO
Kambi
rasmi ya Upinzani Bungeni imesema kuporomoka kwa elimu Nchini pamoja
na sababu nyingi zilizotajwa na Tume mbalimbali za uchunguzi ni
dhahiri kuwa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dkt Shukuru Kawabwa
na Naibu wake Philipo Mulugo wameshindwa kuiongoza wizara hiyo hivyo
hawana budi kujihudhuru
Kauli hiyo imetolewa na Mh Suzani Lyimo(Pichani)
Msemaji Mkuu Kambi rasmi ya Upinzani kwa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya
Ufundi alipokuwa akisoma hotuba ya Makadirio ya mapato na matumizi
kwa mwaka 2013/2014
Katika hotuba yake dakika thelathini Mh Lyimo
ameeleza kuwa kutokana na majanga makubwa yaliyotokea katika Sekta ya
elimu na kusababisha baadhi ya wanafunzi kupoteza uhai Viongozi hao
wataonesha uungwana na uzalendo zaidi kama watawajibika kutokana na
hitilafu zilizojitokea.
Akisoma Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Huduma za Jamii kwa niaba ya Mwenyekiti wa kamati hiyo Mh Zabein
Mhita yeye anafafanua kuwa upungufu wa walimu hasa maeneo ya
Viijjini unasababishwa na Mazingira magumu katika kutekeleza majukumu
yao.
Awali akiwasilisha Makadirio ya mapato na matumizi ya
fedha waziri mwenye dhamana ya Wizara hiyo Dkt shukuru kawambwa
amebainisha yafuatayo.
Wizara hiyo imeomba kutengewa Shilingi Bilioni 689.6 ili kuweza
kutekeleza majukumu yake ,kati ya fedha hizo bilioni 330.1 ni kwa
ajili ya matumizi mengineyo bilioni 188.1 zimetengwa kwa ajili ya
mishahara na bilioni 53.7 zimeobwa kwa ajili ya miradi ya
maendeleo.
JIUNGE NA EDMO BLOG SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube
Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi