WAFA KWA KUNYWA POMBE NYINGI WILAYANI ROMBO

 
Watu wawili wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro wamefariki dunia kwa kile kinachodaiwa kunywa pombe nyingi kupita kiasi. 

Mmoja wa mashuhuda aliyekua na marehemu kabla ya kukumbwa na umauti alisema kuwa marehemu alikunywa pombe za kienyeji, mbege na pombe nyingine na baada ya hapo marehemu aliishiwa nguvu. 

Tukio hilo lilitokea Mnamo tarehe 28juni mwaka huu katika kata ya Shimbi Tarafa ya Mkuu wilayani hapa. 

Wananchi mbalimbali walitoa Maoni yao kuhusiana na matukio hayo huku wakiwatupia lawama viongozi wa vijiji kwa kushindwa kudhibiti suala la ulevi hasa uuzaji wa gongo katika kata hiyo ya Shimbi. 

Suala la ulevi katika wilaya ya Rombo limezidi kushika kasi licha ya juhudi mbalimbali zinafonywa na serikali kudhibiti hali hiyo.

Na, Yohane Gervas, Rombo


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo