VIRUSI VYA HOMA YA DENGUE VYAINGIA NCHINI, WIZARA YA AFYA YATOA TAHADHARI

Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imewatahadharisha wananchi juu ya uwepo wa virusi vya ugonjwa wa homa ya Dengue nchini baada ya kudhibitishwa kwa sampuli za watu waliohisiwa kuwa na ugonjwa huo jijini Dar Es Salaam.

Katika Utafiti uliofanywa na Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu juni 16 mwaka huu ulidhibitisha uwepo wa ugonjwa huo jijini Dar Es Salaam na hadi sasa idadi wa wagonjwa waliogundulika kuwa na dalili za ugonjwa huo ni 20 na hakuna aliyepoteza maisha.

Dkt. Janeth Mghamba ni Kaimu Mkurugenzi Msaidizi Ufuatiliaji wa Magonjwa wa Wizara ya Afya anatoa ufafanuzi juu ya ugonjwa huo ambapo anasema dalili za ugonjwa huo zinafanana na za ugonjwa wa Malaria na hivyo kuwataka wanachi kuchukua tahadhari katika kukabiliana na mbu kwani ndiye anaeneza ugonjwa huo.

Pamoja na hayo wananchi wanashauriwa kutokuwa na hofu juu ya Ugonjwa huo kwani si mara ya kwanza kugunduliwa ambapo Juni 2010, uliripotiwa Jijini Dar es Salaam.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo