TAARIFA YA AWALI KUHUSU MLIPUKO WA BOMU ULIOTOKEA KWENYE MKUTANO WA CHADEMA ARUSHA

DAZANI YA WANACHANA, WAFUASI NA MASHABIKI WA CHADEMA KATIKA MKUTANO WA KUFUNGA KAMPENI ZA UDIWANI SOWETO JIJINI ARUSHA LEO.
WATU wawili wanahofiwa kupoteza maisha na wengine kujeruhiwa kutokana na mlipuko wa bomu lililolipuka kwenye mkutano wa CHADEMA katika eneo la Soweto, kata ya Kaloleni jijini Arusha, wakati wa kufunga kampeni za uchaguzi wa madiwani katika maeneo ya jiji hilo.

Waliojeruhiwa wamekimbizwa katika hospitali ya Seliani na Mount Meru.

Bomu hilo linaelezwa kuwa lilitupwa kwenye mkusanyiko wa watu, lilipuka mwendo wa saa kumi na mbili na robo jioni wakati mkutano huo ulipokuwa umekwisha na shughuli ya kukusanya michango ikiendelea.

Viongozi wa juu wa CHADEMA, Freeman Mbowe na Godbless Lema walikuwepo na wameendelea kuwepo kwenye eneo baada ya mlipuko huo.

Polisi wapo katika eneo hilo wakijitahidi kutuliza ghasia lakini inasemekana upo upinzani mkubwa kutoka kwa wananchi wanaojaribu kuwafukuza, hali iliyowalazimu kupiga mabomu ya machozi na kukamata watu kadhaa wakiwemo viongozi wa CHADEMA.

ILANI: Baadhi ya picha zilizopachikwa hapo huenda zikagusa  hisia yako mtazamaji, tafadhali ikiwa huwezi kuvumilia kuona damu tafadhali usiendelee kuteremka chini ya hapa.
 
CHANZO http://mwanahabariuswazi.blogspot.com
 SEHEMU YA UMATI WA WAFUASI WA CHADEMA KATIKA MKUTANO HUO.WAHANGA WA TUKIO HILO
 
DAMU WANANCHI WAKIANGALIA DAMU ILIYOMWAGIKA KUTOKA KWA WAHANGA HAO.DAMU SAMBAMBA NA KANDAMBILI
GARI LIKIWA LIMEHARIBIWA


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo