Mwili
wa marehemu Albert Mangwea umepelekwa moja kwa moja katika hospitali ya
taifa ya Muhimbili kwa ajili ya kuhifadhiwa mpaka kesho saa 2 asubuhi
wakati ambapo mwili huo utafikishwa katika viwanja vya leaders club na saa 4 asubuhi
shughuli za kuuaga mwili wa marehemu zitafanyika mpaka saa 7 mchana,
Baada
ya hapo utasafirishwa kwenda Morogoro na utalala kwenye nyumba yao na
kesho yake siku ya Alhamisi ndiyo marehemu Albert Mangwea ataagwa tena na
kuzikwa huko Morogoro na hii ndio itakuwa safari ya mwisho ya msanii Albert Mangwea.
Mungu ailaze roho ya marehemu Albert Magwea mahala pema
peponi amina!!!
