Huku
watu wakiwa katika Majonzi ya kupokea mwili wa kipenzi chao mwanamuziki
wa bongo fleva Albert Mangwea kumbe wapo waliokwenda kwa dhamira nyingine
ya Wizi.
Huyu pichani kushoto ni mmoja kati ya vijana hao aliyenusurika kuuwawa na
wananchi wenye majonzi na huzuni kubwa pale alipobainika alikuwa akijaribu kuiba, na kwa bahati nzuri aliokolewa
na Askari wa Ulinzi uwanjani hapo.