skip to main |
skip to sidebar
SIKU YA UGONJWA WA SIKOSELI DUNIANI YAADHIMISHWA JIJINI DAR ES SALAAM LEO
Mwenyekiti
wa Mfuko wa Sikoseli Tanzania, Grace Rubambey (katikati) akizungumza
wakati wa maadhimisho ya Siku ya ugonjwa wa Sikoseli Duniani jijini Dar
es Salaam leo. Wengine kutoka kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Mfuko
huo, Dk Julie Makani, Balozi wa Canada nchini, Alexandre Leveque na
mmoja wa watu wanoishi na ugonjwa huo, Arafa Salim Said.
Balozi wa Canada nchini, Alexandre Leveque (katikati) akizungumza
wakati wa maadhimisho ya Siku ya ugonjwa wa Sikoseli Duniani jijini Dar
es Salaam leo. Wengine kutoka kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Mfuko wa
Sikoseli Tanzania Dk Julie Makani na Mwenyekiti wa mfuko huo, Grace
Rubambey na mmoja wa watu wanoishi na ugonjwa huo, Arafa Salim Said.
Makamu Mwenyekiti wa Mfuko wa Sikoseli Tanzania, Dk Julie Makani
(kushoto) akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya ugonjwa wa
Sikoseli Duniani jijini Dar es Salaam leo. Tanzania ni nchi ya nne
duniani kwa kuwa na idadi kubwa ya watu wanaougua ugonjwa wa sikoseli.
Meneja wa Benki ya KCB Tawi la Msimbazi, Philipo Pilla (kulia)
akizungumza wakati wa maadhjimisho hayo. Benki ya KCB ni mmoja wa
wadhamini wa Mfuko wa Sikoseli Tanzania.
Mratibu
wa Huduma za Ugonjwa wa sikoseli katika Hospitali ya Taifa Muhimbili
Dk. Deogratias Soka (kulia) akizungumza kuhusu hali ya ugonjwa huo
katika hospitali hiyo katika maadhimisho hayo. Inakadiriwa kuwa katika
ya watoto 8,000 hadi 10,000 kuzaliwa na ugonjwa huo nchini Tanzania kila
mwaka.
Baadhi
wa watu walioshiriki maadhimisho jijini Dar es Salaam leo. Ugonjwa wa
sikoseli ni ugonjwa wa kurithi unaosababisha mabadiliko yasiyo ya
kawaida katika chembechembe nyekundu za damu hivyo mtu hawezi
kuambukizwa kwa njia yoyote ile kama vile kuishi au kuwa karibu na
mgonjwa wa sikoseli.
JIUNGE NA EDMO BLOG SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube
Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi