PICHA ZA MAADHIMISHO YA SIKU YA MTOTO WA AFRIKA IPELELE WILAYANI MAKETE

 Watoto wawili Zaifa Daudi na Nobi Sadiki ambao wanaishi katika mazingira hatarishi kwa tabu zaidi katika kata ya Ipelele wilayani Makete ambao waligundulika na shirika la ELCT Makete kupitia programu ya pamoja tuwalee wakijitokeza mbele ili watu wawaone katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa afrika wilaya ya Makete yaliyofanyika katika kata ya Ipelele
 Watoto wakisikiliza kwa makini kuhusu watoto wenzao wanaoishi katika mazingira hatarishi
Mwanamuziki Aldo Sanga (kulia)akiimba wimbo wake wa jipe moyo katika maadhimisho hayo
Watoto wakiimba ngonjera
wazazi wakishuhudia watoto wao wakiimba
Meza kuu ikisikiliza kwa makini nyimbo zinazoimbwa na watoto
 Mkuu wa wilaya ya Makete Josephine Matiro ambaye pia alikuwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo akimfariji mtoto yatima ambaye alimwaga machozi baada ya kusikia Aldo Sanga akiimba wimbo wake wa jipe moyo
Mratibu wa programu ya pamoja tuwalee Mch. Ezekiel Sanga akielezea namna programu ya pamoja tuwalee inavyofanya kazi pamoja na kuomba kuungwa mkono na wananchi kuwachangia watoto wawili wenye matatizo zaidi na wanaishi katika mazingira hatarishi 
Mkuu wa wilaya ya makete Josephine Matiro akimkabidhi afisa mtendaji wa kata ya Ipelele Anna Sanga jumla ya sh.282,500/= zilizochangwa kwa ajili ya kuwasaidia watoto Zaifa na Nobi ambao wanaishi katika mazingira hatarishi zaidi
watoto wakisoma risala kwa mgeni rasmi
 Mgeni rasmi akikabidhiwa risala
 Mkuu wa wilaya ya makete Josephine Matiro akikabidhi zawadi kwa watoto waishio katika mazingira hatarishi
Mkuu wa wilaya akihutubia wananchi wa Ipelele waliohudhuria maadhimisho ya siku ya mtoto wa afrika
 mama huyu alishindwa kujizuia na kuamua kulisakata rumba kwenya maadhimisho hayo
Watoto wote 60 waliopatiwa zawadi pia walipata wasaa wa kupiga picha ya pamoja na mgeni rasmi
wakati maadhimisho yakiendelea pia na biashara zilichanganya balaaa
Mgeni rasmi ambaye ni mkuu wa wilaya ya makete Josephine Matiro akiondoka eneo la tukio mara baada ya maadhimisho kufikia tamati


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo