Nairobi, Kenya. Ukitaka kumfahamu mtu, tazama aina ya watu
wanaomzunguka. Msemo huu unaweza kutumika kuielezea Tanzania hasa baada
ya kupata fursa ya kutembelewa na marais watatu wa taifa lenye nguvu
zaidi duniani, Marekani.
Kwa mara ya kwanza, Tanzania ilitembelewa na Rais wa Marekani aliyeko
madarakani, George W Bush mwanzoni mwa 2008 na sasa nchi imepata fursa
tena ya kutembelewa na rais mwingine wa nchi hiyo, Barack Obama ambaye
atakuwa ameambatana tena na Bush, jambo ambalo ni la kihistoria katika
Bara la Afrika.
Pamoja na kwamba kuna hali ya kutoridhika na hali
halisi ya nchi, kiuchumi, kisiasa na kijamii kutoka kwa baadhi ya
Watanzania, hali inaonekana kuwa ni tofauti kabisa kwa Marekani ambayo
mtazamo wake wa masuala ya nchi za nje unawakilisha mtazamo wa mataifa
mengi ya magharibi.
Akizungumzia sababu za ziara hiyo kwa njia ya
conference call kutoka Washington, Naibu Mshauri wa Masuala ya Ulinzi wa
Ikulu ya Marekani, Gayle Smith alisema Obama anazuru Tanzania kwa
sababu nchi hiyo ni rafiki mkuu wa Marekani katika Afrika Mashariki na
kwamba imebobea katika misingi ya kidemokrasia.
Smith alisema Bara
la Afrika hususan Tanzania ni moja ya masoko muhimu sana yanayoibukia
ulimwenguni na Marekani ni lazima iongeze harakati zake barani humo.
“Kuna
fursa nyingi za kiuchumi, biashara na uwekezaji jambo ambalo linaitisha
umuhimu wa kampuni na biashara za Marekani kujikita zaidi Afrika,”
anasema Smith.
Tofauti na ziara ya Bush ambayo ililenga zaidi
kuisaidia Tanzania kutoa huduma bora kwa watu wake hususan afya; ziara
ya Obama imetokana na maombi na msukumo kutoka kwa wafanyabiashara wa
Marekani ambao waliitaka Serikali yao kuunda mikakati ya makusudi ya
kuhakikisha nchi hiyo inakuza na kuboresha uhusiano wa kibiashara na
Waafrika.
Wakati wa ziara ya George W Bush, Tanzania ilinufaika na
msaada wa dola 698 milioni kwa ajili ya ununuzi wa vyandarua na dawa za
kuulia mbu pamoja na kuendeleza mapambano dhidi ya Ukimwi.
Maambukizi ya Ukimwi yalianza kushuka mwaka 2008 kutoka asilimia saba mwaka 2003 hadi kufikia asilimia tano na mwaka huu.
Idadi
ya watu ambao wanajitokeza kupimwa Ukimwi na kuchukua majibu yao
imeongezeka kutoka asilimia 20 ya wanawake mwaka 2008 hadi kufikia
asilimia 30 mwaka 2012 na kwa wanaume imepanda kutoka asilimia 19 mwaka
huohuo na kufikia asilimia 27 mwaka 2012.
Kwa upande wa malaria,
kaya tisa kati ya 10 zinatumia vyandarua vyenye dawa ongezeko ambalo ni
mara nne zaidi ya idadi ya kaya zilizotumia vyandarua hivyo mwaka 2004.
Hali
kadhalika, zaidi ya asilimia 70 ya watoto ambao wako hatarini
kuambukizwa malaria walilala ndani ya vyandarua ongezeko ambalo pia ni
mara nne zaidi ya idadi ya mwaka 2004.Inaendelea… Bofya hapa kusoma zaidi