Naibu
katibu mkuu wa CCM Mh.Mwigulu nchemba akihutubia mamia ya wakazi wa
jiji la Arusha kata ya Kimandolu kwenye kampeni za uchaguzi mdogo wa
udiwani.Mh.Mwigulu nchemba amesisitiza kudumisha Amani ndani ya jiji la
Arusha,Amewasihi wanaarusha kuacha kushabikia vyama vinavyofurahia na
kuhubiri vurugu siku zote."Wanaarusha kufanya uchaguzi mdogo wa udiwani
si kubadirisha serikali,Serikali itabaki ileile ya CCM na sera zitabaki
zilezile za CCM,tunachokifanya hapa ni kuongeza nguvu ilikurejesha
heshima ya chama cha mapinduzi na jiji la Arusha.Kumekuwa na sifa mbaya
kwamba Arusha sikuhizi hakuana amani,daladala zinasurutishwa kugoma
ilimradi tu mbunge wa CHADEMA Godbless Lema asikike kwamba leo ameleta
vurugu.WanaArusha sifa za kijinga zimepitw ana wakati,fanyeni chaguo
sahihi kwa kumchagua Bi.Edna Saul kuwa diwani wa CCM kata ya kimandolu |