NAPE AITAKIA USHINDI MNONO TAIFA STARS

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeitakia kila la kheri timu ya Taifa Stars ambayo inacheza  kutafuta tiketi ya kucheza kombe la dunia mwaka 2014.

Taifa Stars katika mechi yake ya kesho itavaana na Timu ya taifa ya Morocco. 

Akizungumza kutoka Dar es salaam ,Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndg. Nape Nnauye alisema CCM inaitakia kila lakheri Taifa Stars na mafanikio katika mchezo wa kesho na kwamba CCM inatambua umuhimu wa taifa Stars kushinda mechi hiyo ya kesho.


Alisema anaamini dua za CCM na Watanzania wote zitaiwezesha Taifa Stars  kushinda mechi yake dhidi ya Morocco."Watanzania tunaomba muiombee Taifa Stars, tunaimani nayo, bila shaka itashinda kesho" alisisitiza Nape


Nape Moses Nnauye
The CCM Secretary for Ideology & Publicity


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo