KESI YA LADY JAYDEE YAPIGWA TENA KALENDA


Kesi ya mwanamuziki, Judith 'Lady JayDee' Wambura, imeahirishwa mpaka tarehe 30 Julai, 2013.

Kwa mujibu wa wakili wa Lady JayDee, Bw. Mabere Nyaucho Marando, kesi hiyo imeahirishwa kwa sababu upande uliofungua mashtaka haukutokea mahakamani, na wala kutoa taarifa yoyote: “Kesi haiwezi kusikilizwa kama hawakutokea,” alisema Marando.

Kesi ya madai iliyofunguliwa na uongozi wa Clouds Media Group, ilikuwa isikilizwe leo kutokana na maombi ya kuwa iharakishwe lakini upande wa Clouds Media hawakutokea.

Lady JayDee kama kawaida yake aliwasili katika Mahakama ya Kinondoni saa tano kasoro kumi akifuatana na mumewe Gardner G Habash na kuelekea moja kwa moja chumba cha mahakamani. Waandishi wa habari hawakuruhusiwa kuingia ndani.

Anatuhumiwa za kuwachafua viongozi wa Clouds Media Group, Joseph Kusaga na Ruge Mutahaba.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo