Aminiel Aligaesha ambae ni Afisa Uhusiano wa hospitali ya
Taifa Muhimbili amethibitisha kwamba msanii Langa amefariki dunia June
13 2013 saa kumi na moja jioni baada ya kufikishwa hospitalini hapo toka
juzi jioni ambapo kutokana na sababu za kimaadili kwenye tiba,
Muhimbili hospitali hawawezi kusema rapper huyu alikua anaumwa nini bali
ndugu ndio wenye mamlaka ya kufanya hivyo.
Kwenye maelezo aliyoyatoa Aminiel amesema
Marehemu Langa alipokelewa kwenye idara ya wagonjwa wa magonjwa ya
dharura usiku wa kuamkia jana na kupatiwa huduma ambapo leo June 13 2013
ndio alihamishiwa kwenye chumba cha wagonjwa Mahututi na baadae
kufariki dunia.
