Mkuu wa upelelezi(OCCID) wilaya ya Makete Gosbert Komba
========
Jeshi la polisi wilaya ya Makete mkoani Njombe linamshikilia
msichana anayesoma kidato cha tatu katika shule ya sekondari Kitulo (jina
linahifadhiwa kwa sasa) kwa tuhuma za kutoa mimba ya miezi minne
Akizungumza na ripota wetu Mkuu wa upelelezi wilaya ya
makete Bw Gosbert Komba amesema wanamshikilia mwanafunzi huyo baada ya kupatiwa
taarifa za kutenda kosa hilo ambalo ni kinyume na sheria za nchi
Amesema wamepata taarifa za msichana huyo kutoa mimba kutoka
kwa mwalimu mkuu wa shule hiyo ambapo baada ya mahojiano baina ya polisi na
binti huyo, alikiri kutenda kosa hilo
Akizungumzia sakata hilo binti huyo amesema ni kweli ametoa
ujauzito huo kwa kutumia vidonge ambavyo hakueleza amevipata wapi ama
ameshauriwa na nani kutenda kosa hilo ambapo pia kwa mujibu wa maelezo yake ana
kijutia kitendo hicho alichokifanya
“Mimi ni kweli nimetoa mimba na baada ya kufanya hivyo
naatamani sana kurudi shuleni kuendelea na masomo, sitaangalia jamii itanielewa
vipi ama wanafunzi wenzangu pale shuleni lakini pia zaidi ya yote najutia
kitendo nilichokifanya” alisema mwanafunzi huyo wakati akihojiwa na polisi
Amedai kuwa mwanaume aliyempa ujauzito huo amemaliza kidato
cha 6 kwa sasa na walianza uhusiano wa kimapenzi tangu januari mwaka huu na alipogundua kuwa amempa mimba mwanafunzi huyo jamaa ametoroka
Kwa mujibu wa jeshi la polisi Makete mwanafunzi huyo
anatarajiwa kufikishwa mahakamani kujibu shitaka linalomkabili muda wowote
kuanzia sasa, huku Bw. Komba akikiri kuwepo kwa vitendo vya utoaji mimba
wilayani hapo ambavyo hufanyika kwa siri kubwa