HII NDIYO AIRTEL TANZANIA BWANA


 Airtel Tanzania imeendelea kutimiza dhamira yao ya kuwapatia wateja wake unafuu zaidi kupitia huduma yake ya AIRTEL YATOSHA nchini ambapo sasa wateja watafurahia Vifurushi vya Airtel Yatosha kwa masaa 25 kwa siku,   hii itawawezesha watanzania kufurahia kupiga simu mtandao wowote kwa gharama nafuu kwa muda mrefu zaidi.

Akiongea wakati wa uzinduzi wa Airtel yatosha masaa 25 Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando alisema” kuanzia sasa, huduma ya Airtel yatosha kwa siku itakua kwa masaaa 25 kuanzia pale mteja anapojiunga na huduma, yaani masaa 24 ya kuongea na kama vile haitoshi Airtel yatosha inakuongezea saa jingine moja la ziada. Sasa wateja wa Airtel watafurahi kupiga simu kwa gharama nafuu na kwa muda zaidi kuliko ilivyokuwa awali”.

 “Hii ni ya kwanza na pekee kutoka Airtel, Airtel yatosha itaendelea kuwa suluhisho la mawasiliano ya huduma za simu kwa watumiaji na wateja wa Airtel nchi nzima”. aliongeza Mmbando

Airtel yatosha ni huduma iliyoanzishwa ili kuleta kuvunja mipaka kwa watanzania na kuwawezesha kuwasiliana ndani na nje ya mtandaa kwa gharama nafuu. Kujiunga na huduma hii  piga *149*99# na Utapata majibu papo hapo Uchague unataka Yatosha WIKI au Yatosha SIKU au Tosha ya Mwezi.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo