BREAKING NEWS: MAHAKAMA YAMWACHIA HURU IDDI SIMBA

Na Happiness Katabazi
 
HATIMAYE Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, hivi punde imemwachiria huru Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA), Idd Simba, Mkurugenzi wa Bodi hiyo ambaye alikuwa Diwani wa Kata Sinza(CCM), Salum Mwaking’inda, Meneja Mkuu wa shirika hilo Victor Milanzi na Mkurugenzi wa Kampuni ya Simon Group , Simon Kisena waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi wa shirika hilo kwa sababu Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), Dk.Eliezer Feleshi kuwasilisha hati ya kutokuwa na haja ya kuendelea kuwashitaki washitakiwa hao chini ya kifungu cha 91(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya mwaka 2002. 

Simba anayetetewa na wakili maarufu nchini Alex Mgongolwa walifikishwa na mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Mei 27 mwaka jana wakikabiliwa na makosa ya kula njama,matumizi mabaya ya madaraka na kughushi na hujumu uchumi. 

Hivyo kuanzia sasa washitakiwa hao wapo huru.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo